Utata wa ardhi wakumba ujenzi wa reli mpya Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Ujenzi wa reli mpya wazua utata Kenya

Katika sehemu ya pili leo kuhusu utata uliozuka wa ujenzi wa reli ya kisasa sehemu ya Voi na Maungu kaunti ya Taita-Taveta, eneo la pwani ya Kenya, tume ya kitaifa ya ardhi imejitetea kuhusu shutuma za kuwanyanyasa wakaazi huko kwa malipo ya fidia ya ardhi yao itakayotumika kwa mradi huo.

Naye Gavana wa kaunti hiyo John Mrutu ameilaumu tume hiyo ya ardhi kwa kuwapa kisogo.

Reli hiyo itaanzia Mombasa hadi Uganda na Rwanda……John Nene anatupasha zaidi…